Matthew 11

1Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao, 2na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake, 3na wakamuuliza, “Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?”

4Yesu akajibu na kusema kwao “Nendeni mkamtaarifu Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia. 5Watu wasioona wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, watu wasiosikia wanasikia tena, watu waliokufa wanafufuliwa kupata uhai, na watu wahitaji wanahubiriwa habari njema. 6Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.

7Pindi watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, “Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa __tete likitikiswa na upepo? 8Lakini nini mlikwenda kuona__mtu aliyevaa mavazi mololo? Hakika, wale wavaao mavazi mololo hukaa katika nyumba za wafalme.

9Lakini mliondoka kuona nini-Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii. 10Huyu ndiye aliyeandikiwa, ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.

11Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye. 12Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.

13Kwa kuwa manabii na sheria, ikamelcuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana. 14Na kamamko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye. 15Aliye na masikio ya kusikia na asikie.

16Nikilinganishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana 17na kusema, ‘Tuliwapigia zomari na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.’

18Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, ‘Ana pepo.’ 19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema ‘Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!’ Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.‘’

20Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu, 21Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yangetendeka Tiro na Sidoni yale yaliyotendeka hapa, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. 22Lakini itakuwa uvumilivu kwa Tiro na Sidoni siku ya hukumu kuliko kwako.

23Wewe, Kapernaum, unadhani utainuliwa hadi mbinguni? Hapana utashushwa hadi chini kuzimu. Kama kwa Sodoma kungefanyika matendo makuu, kama yalifanyika kwako, ingekuwepo hadi leo. 24Bali nasema kwako kwamba itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoma kusimama siku ya hukumu kuliko wewe.

25Katika muda huo Yesu alisema, “Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyafunua kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo. 26Baba kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako. 27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.

28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

30

Copyright information for SwaULB