‏ 1 Kings 7:15-22

15 aHiramu akasubu nguzo mbili za shaba, kila moja ikiwa na urefu wa dhiraa kumi na nane,
Dhiraa 18 ni sawa na mita 8.1.
kila nguzo ikiwa na mzingo wa dhiraa kumi na mbili
Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4.
kwa mstari.
16 dPia alitengeneza mataji mawili ya shaba ya kusubu ili kuyaweka juu ya hizo nguzo; kila taji lilikuwa na kimo cha dhiraa tano
Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.
kwenda juu.
17 fWavu wa mikufu iliyosokotewa kwenye zile taji juu ya zile nguzo, saba kwa kila taji. 18Akatengeneza makomamanga katika safu mbili kuzunguka kila wavu kuremba mataji yaliyo juu ya nguzo. Alifanya hivyo kwa kila nguzo. 19 gMataji yaliyokuwa juu ya nguzo kwenye baraza, yalikuwa katika umbo la yungiyungi, kimo chake ni dhiraa nne
Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.
20 iJuu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga 200 katika safu kuzunguka pande zote. 21 jHiramu akasimamisha nguzo kwenye baraza ya Hekalu. Nguzo ya upande wa kusini akaiita Yakini,
Yakini maana yake Mungu atafanya imara.
na ile ya upande wa kaskazini Boazi.
Boazi maana yake Ndani ya Mungu kuna nguvu.
22Mataji yaliyokuwa juu yalikuwa na umbo la yungiyungi. Hivyo kazi ya nguzo ikakamilika.

Copyright information for SwhNEN