bKum 12:5; 1Fal 5:5; 6:12; 8:19, 29; Kum 16:11; 2Fal 21:4, 7; Mit 25:5; Dan 7:27; Mwa 9; 16; 2Sam 22:51; 1Fal 2:4, 45; 1Nya 22; 10; 28:6; 2Nya 6:16; 7:18; 13:5; 21:7; Za 89:3-4; Isa 9:7; 16:5; Yer 17:25; 33:17-21
2 Samuel 7:12-16
12 aSiku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake. 13 bYeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele. 14 cNitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu. 15 dLakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako. 16Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”
Copyright information for
SwhNEN