Exodus 36:8-38
Maskani Ya Mungu
(Kutoka 26:1-37)
8 aWatu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. 9Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane, ▼▼Dhiraa 28 ni sawa na mita 12.6.
na upana wa dhiraa nne ▼▼Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.
10Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. 11Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. 12 dWakatengeneza pia vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vikaelekeana. 13Kisha wakatengeneza vifungo hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha zile fungu mbili za mapazia pamoja ili maskani ipate kuwa kitu kimoja. 14 eWakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. 15Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini, ▼
▼Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.
na upana wa dhiraa nne. 16Wakaunganisha mapazia matano kuwa fungu moja, na hayo mengine sita kuwa fungu lingine. 17Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. 18Wakatengeneza vifungo hamsini vya shaba ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. 19 gKisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo. ▼▼Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.
20 iWakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 21Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi, ▼
▼Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
na upana wa dhiraa moja na nusu, ▼▼Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.
22zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 23Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 24na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 25Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini 26na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. 27Wakatengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, 28na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za maskani za upande uliokuwa mbali. 29 lKatika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana. 30Kwa hiyo kulikuwa na mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. 31 mWakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, 32matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. 33Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. 34Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika hayo mataruma kwa dhahabu.
35 nWakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye hilo pazia. 36Wakatengeneza nguzo nne za mti wa mshita kwa ajili yake na kuzifunika kwa dhahabu. Wakatengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya nguzo hizo, na kusubu vitako vinne vya fedha. 37 oKwa ajili ya ingilio la hema wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. 38 pPia wakatengeneza nguzo tano zenye kulabu. Wakafunika ncha za juu za hizo nguzo pamoja na tepe zake kwa dhahabu, na pia wakatengeneza vitako vyake vitano vya shaba.
Copyright information for
SwhNEN