Isaiah 12:1-3
Kushukuru Na Kusifu
1 aKatika siku ile utasema:“Nitakusifu wewe, Ee Bwana.
Ingawa ulinikasirikia,
hasira yako imegeukia mbali
nawe umenifariji.
2 bHakika Mungu ni wokovu wangu;
nitamtumaini wala sitaogopa.
Bwana, Bwana, ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu.”
3 cKwa furaha mtachota maji
kutoka visima vya wokovu.
Copyright information for
SwhNEN