b Kum 32:6; Kut 15:17; Yer 2:21; Mt 21:19; Mk 11:13; Isa 16:8; 27:3; 1Sam 2:9; Ay 24:11; Mt 21:33; Lk 13:6
Isaiah 5:1-7
Wimbo Wa Shamba La Mizabibu
1 aNitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye,kuhusu shamba lake la mizabibu:
Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu
kwenye kilima chenye rutuba.
2 bAlililima na kuondoa mawe
na akaliotesha mizabibu bora sana.
Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake,
na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia.
Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri,
lakini lilizaa matunda mabaya tu.
3 c“Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda,
hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu.
4 dNi nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibu
kuliko yale niliyofanya?
Nilipotazamia kupata zabibu nzuri,
kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu?
5 eSasa nitawaambia lile nitakalolitendea
shamba langu la mizabibu:
Nitaondoa uzio wake,
nalo litaharibiwa,
nitabomoa ukuta wake,
nalo litakanyagwa.
6 fNitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu,
halitakatiwa matawi wala kulimwa,
nayo michongoma na miiba itamea huko,
nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.”
7 gShamba la mzabibu la Bwana Mwenye Nguvu Zote
ni nyumba ya Israeli,
na watu wa Yuda
ni bustani yake ya kumpendeza.
Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu,
alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu.
Copyright information for
SwhNEN