aHes 13:29; Amu 10:11; 11:26; Amo 2:10; Hes 32:3; Kum 1:4; 29:7; Yos 9:10; 12:2; Isa 15:4; 16:8; Yer 48:2
d Hes 24:17; 2Sam 8:2; 1Nya 18:2; Za 60:8; Isa 25:10; Yer 48:46; Amu 10:6; 11:24; Rum 1:15; 1Fal 11:7; 2Fal 23:13; Yer 48:7; Isa 15:5; 16:2
g Yos 2:1; 6:22; 7:2; Amu 18:2; 2Sam 10:3; 1Nya 19:3; Hes 32:1; Yos 13:25; 2Sam 24:5; 1Nya 6:8; Isa 16:8; Yer 48; 32
Numbers 21:25-35
25 aIsraeli akaiteka miji yote ya Waamori na kuikalia, pamoja na Heshboni na makazi yote yanayoizunguka. 26 bHeshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.27Ndiyo sababu watunga mashairi husema:
“Njoo Heshboni na ujengwe tena;
mji wa Sihoni na ufanywe upya.
28 c“Moto uliwaka kutoka Heshboni,
mwali wa moto kutoka mji wa Sihoni.
Uliteketeza Ari ya Moabu,
raiya wa mahali pa Arnoni palipoinuka.
29 dOle wako, ee Moabu!
Umeharibiwa, enyi watu wa Kemoshi!
Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,
na binti zake kama mateka
kwa Mfalme Sihoni wa Waamori.
30 e“Lakini tumewashinda;
Heshboni umeharibiwa hadi Diboni.
Tumebomoa hadi kufikia Nofa,
ulioenea hadi Medeba.”
31 fKwa hiyo Israeli akaishi katika nchi ya Waamori.
32 gBaada ya Mose kutuma wapelelezi kwenda mji wa Yazeri, Waisraeli waliteka viunga vya mji huo na kuwafukuza Waamori waliokuwa wanaishi huko. 33 hKisha wakageuka na kwenda katika njia inayoelekea Bashani, naye Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote wakatoka kupigana nao huko Edrei.
34 i Bwana akamwambia Mose, “Usimwogope Ogu, kwa sababu nimeshamkabidhi mikononi mwako, pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Mtendee kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”
35 jKwa hiyo wakamuua, pamoja na wanawe na jeshi lake lote, bila ya kumwacha hata mtu mmoja hai. Nao wakaimiliki nchi yake.
Copyright information for
SwhNEN