a Za 9:9; 18:1, 6; 25:17; 34:18; 61:3; 37:39; 73:26; 91:2, 9; 142:5; Isa 33:16; Lk 1:54; Yer 16:19; 17:17; Yoe 3:16; Nah 1:7; Mao 3:57; Kum 4:30
Psalms 46:1-5
Mungu Yuko Pamoja Nasi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi.
1 aMungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 bKwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa
nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.
3 cHata kama maji yake yatanguruma na kuumuka,
milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.
4 dKuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu,
mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.
5 eMungu yuko katikati yake, hautaanguka,
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
Copyright information for
SwhNEN