‏ Psalms 68

Wimbo Wa Taifa Wa Shangwe Kwa Ushindi

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.

1 aMungu na ainuke, watesi wake watawanyike,
adui zake na wakimbie mbele zake.
2 bKama vile moshi upeperushwavyo na upepo,
vivyo hivyo uwapeperushe mbali,
kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto,
vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu.
3 cBali wenye haki na wafurahi,
washangilie mbele za Mungu,
wafurahi na kushangilia.

4 dMwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake,
mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu:
jina lake ni Bwana,
furahini mbele zake.
5 eBaba wa yatima, mtetezi wa wajane,
ni Mungu katika makao yake matakatifu.
6 fMungu huwaweka wapweke katika jamaa,
huwaongoza wafungwa wakiimba,
bali waasi huishi katika nchi kame.

7 gEe Mungu, ulipowatangulia watu wako,
ulipopita nyikani,
8 hdunia ilitikisika,
mbingu zikanyesha mvua,
mbele za Mungu, Yule wa Sinai,
mbele za Mungu, Mungu wa Israeli.
9 iEe Mungu, ulinyesha mvua nyingi
na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka.
10 jEe Mungu, watu wako waliishi huko,
nawe kwa wingi wa utajiri wako
uliwapa maskini mahitaji yao.

11 kBwana alitangaza neno,
waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:
12 l“Wafalme na majeshi walikimbia upesi,
watu waliobaki kambini waligawana nyara.
13 mHata ulalapo katikati ya mioto ya kambini,
mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha,
manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.”
14 nWakati Mwenyezi
Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.
alipowatawanya wafalme katika nchi,
ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni.

15Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka,
milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka.
16 pEnyi milima yenye vilele vilivyochongoka,
kwa nini mnakazia macho kwa wivu,
katika mlima Mungu anaochagua kutawala,
ambako Bwana mwenyewe ataishi milele?
17 qMagari ya Mungu ni makumi ya maelfu,
na maelfu ya maelfu;
Bwana amekuja kutoka Sinai
hadi katika patakatifu pake.
18 rUlipopanda juu, uliteka mateka,
ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu,
hata kutoka kwa wale walioasi,
ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko.

19 sSifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu,
ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.
20 tMungu wetu ni Mungu aokoaye,
Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo.

21 uHakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake,
vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi.
22 vBwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani;
nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari,
23 wili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako,
huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.”

24 xEe Mungu, maandamano yako yameonekana,
maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu,
yakielekea patakatifu pake.
25 yMbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda,
pamoja nao wako wanawali wakipiga matari.
26 zMsifuni Mungu katika kusanyiko kubwa,
msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli.
27 aaLiko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza,
wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda,
hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali.

28 abEe Mungu, amuru uwezo wako,
Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako,
kama ulivyofanya hapo awali.
29 acKwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu
wafalme watakuletea zawadi.
30 adMkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi,
kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa.
Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea.
Tawanya mataifa yapendayo vita.
31 aeWajumbe watakuja kutoka Misri,
Kushi
Kushi hapa ina maana maeneo ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.
atajisalimisha kwa Mungu.

32 agMwimbieni Mungu, enyi falme za dunia,
mwimbieni Bwana sifa,
33 ahmwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu,
yeye angurumaye kwa sauti kuu.
34 aiTangazeni uwezo wa Mungu,
ambaye fahari yake iko juu ya Israeli,
ambaye uwezo wake uko katika anga.
35 ajEe Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako,
Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu.

Mungu Asifiwe!
Copyright information for SwhNEN