‏ Psalms 88

Kilio Kwa Ajili Ya Kuomba Msaada

Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi.

1 aEe Bwana, Mungu uniokoaye,
nimelia mbele zako usiku na mchana.
2Maombi yangu yafike mbele zako,
utegee kilio changu sikio lako.

3 bKwa maana nafsi yangu imejaa taabu,
na maisha yangu yanakaribia kaburi.
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

4 dNimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni,
niko kama mtu asiye na nguvu.
5 eNimetengwa pamoja na wafu,
kama waliochinjwa walalao kaburini,
ambao huwakumbuki tena,
ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.

6 fUmenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana,
katika vina vya giza nene.
7 gGhadhabu yako imekuwa nzito juu yangu,
umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.

8 hUmenitenga na rafiki zangu wa karibu
na kunifanya chukizo kwao.
Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;
9 inuru ya macho yangu
imefifia kwa ajili ya huzuni.

Ee Bwana, ninakuita kila siku,
ninakunyooshea wewe mikono yangu.
10 jJe, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako?
Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?

11 kJe, upendo wako hutangazwa kaburini,
uaminifu wako katika Uharibifu?
Yaani Abadon.

12 mJe, maajabu yako hujulikana mahali pa giza,
au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?

13 nLakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie;
asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
14 oEe Bwana, kwa nini unanikataa
na kunificha uso wako?

15 pTangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo;
nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.
16 qGhadhabu yako imepita juu yangu;
hofu zako zimeniangamiza.
17 rMchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko;
zimenimeza kabisa.
18 sUmeniondolea marafiki na wapendwa wangu;
giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.
Copyright information for SwhNEN