f Flp 2:10; Efe 3:14; 2Nya 6:13; 1Kor 6:20; 2Sam 12:16; Za 22:29; 100:3; 149:2; Lk 22:41; Isa 17:7; 54:5; Dan 6:10, 11; Ezr 9:5; 1Fal 8:54; Hos 8:14; Yn 1:3; Ay 35:10
Psalms 95
Wimbo Wa Kumsifu Mungu
1 aNjooni, tumwimbie Bwana kwa furaha;tumfanyie kelele za shangwe
Mwamba wa wokovu wetu.
2 bTuje mbele zake kwa shukrani,
tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3 cKwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4 dMkononi mwake mna vilindi vya dunia,
na vilele vya milima ni mali yake.
5 eBahari ni yake, kwani ndiye aliifanya,
na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 fNjooni, tusujudu, tumwabudu,
tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,
7 gkwa maana yeye ndiye Mungu wetu,
na sisi ni watu wa malisho yake,
kondoo chini ya utunzaji wake.
Kama mkiisikia sauti yake leo,
8 hmsiifanye mioyo yenu migumu
kama mlivyofanya kule Meriba, ▼
▼Meriba maana yake ni Kugombana.
kama mlivyofanya siku ile
kule Masa ▼
▼Masa maana yake ni Kujaribiwa.
jangwani,9 kambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.
10 lKwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,
nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,
nao hawajazijua njia zangu.”
11 mHivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,
“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
Copyright information for
SwhNEN