‏ Zechariah 11

1 aFungua milango yako, ee Lebanoni,
ili moto uteketeze mierezi yako!
2 bPiga yowe, ee mti wa msunobari,
kwa kuwa mwerezi umeanguka;
miti ya fahari imeharibiwa!
Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,
msitu mnene umefyekwa!
3 cSikiliza yowe la wachungaji;
malisho yao manono yameangamizwa!
Sikia ngurumo za simba;
kichaka kilichostawi sana
cha Yordani kimeharibiwa!

Wachungaji Wawili Wa Kondoo

4 dHili ndilo asemalo Bwana Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. 5 eWanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwana asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. 6 fKwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema Bwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”

7 gKwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi. 8 hKatika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu.

Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao,
9 inikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.”

10 jKisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote. 11Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la Bwana.

12 kNikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.

13 lNaye Bwana akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya Bwana.

14Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli!

15Kisha Bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.

17 m“Ole wa mchungaji asiyefaa,
anayeliacha kundi!
Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume!
Mkono wake na unyauke kabisa,
jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”
Copyright information for SwhNEN