o Mal 1:6; Kut 21:17; Law 19:3; Eze 22:7; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2-3; Kum 4:40; 11:9; Mit 3:1-2
p Mwa 9:6; Law 24:17; Mhu 3:3; Yer 40:15; 41:3; Mt 5:21-22; 19:19; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11
ab Za 81:8, 13; Yos 22:5; Za 78:7; Kum 4:1-40; 12:25; 22:7; Isa 48:18; Kum 12:25; Yer 44:4; Mt 23:37; Lk 19:42; 2Kor 5:20; 6:1; 7:1; Ebr 12:25; Yn 15:14; Ufu 22:14
Deuteronomy 5
Amri Kumi
(Kutoka 20:1-17)
1 aMusa akawaita Israeli wote, akawaambia: Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. 2 b Bwana Mwenyezi Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 3 cSi kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 4 d Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 5 e(Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema: 6 f“Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.7 gUsiwe na miungu mingine ila mimi.
8 hUsijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. 9 iUsivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mwenyezi Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10 jlakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
11 kUsilitaje bure jina la Bwana Mwenyezi Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.
12 lAdhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama Bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokuagiza. 13Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. 14 mLakini siku ya Saba ni Sabato kwa Bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ng’ombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe. 15 nKumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo Bwana Mwenyezi Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.
16 oWaheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi Bwana Mwenyezi Mungu wako anayokupa.
17 pUsiue.
18 qUsizini.
19 rUsiibe.
20 sUsimshuhudie jirani yako uongo.
21 tUsitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ng’ombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”
22 uHizi ndizo amri alizozitangaza Bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.
Uoga Wa Watu Mlimani
(Kutoka 20:18-21)
23 vMliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 24 wNanyi mkasema, “Bwana Mwenyezi Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 25 xLakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu wetu zaidi. 26 yNi mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 27 zSogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mwenyezi Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mwenyezi Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.” 28 aa Bwana aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na Bwana akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri. 29 abLaiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele! 30 ac“Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao. 31 adLakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.” 32 aeHivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto. 33 afFuateni yale yote ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
Copyright information for
SwhKC