i Kut 3:7; 5:4, 10-14; 6:6-7; 2:11; Mwa 15:13; 47:11; Yos 9:27; Isa 60:10; 1Fal 9:19, 21; 1Nya 22:2; 2Nya 8:4
Exodus 1
Waisraeli Waonewa
1 aHaya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake: 2Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; 3Isakari, Zabuloni na Benyamini; 4 bDani na Naftali, Gadi na Asheri. 5 cWazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yusufu alikuwa tayari yuko Misri. 6 dBasi Yusufu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, 7 elakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi. 8 fKisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yusufu akatawala Misri. 9 gAkawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi. 10 hNjooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.” 11 iBasi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao. 12Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli, 13 jkwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili. 14 kWakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili. 15 lMfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, 16“Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” 17 mLakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. 18Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?” 19 nWakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.” 20 oKwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. 21 pKwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe. 22 qKisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”
Copyright information for
SwhKC