Exodus 38
Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa
(Kutoka 27:1-8)
1 aAkatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu; ▼▼ Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.
nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wa dhiraa tano ▼▼ Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.
2 dAkatengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu zikawa zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. 3 eAkatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama na vyombo vya kuchukulia moto. 4Akatengeneza wavu wa shaba chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 5Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya zile pembe nne za huo wavu wa shaba. 6Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba. 7Akaiingiza ile mipiko kwenye zile pete, ili iwe pande mbili za madhabahu kwa ajili ya kuibeba. Akaitengeneza madhabahu yenye uvungu ndani yake akitumia mbao. Sinia La Kunawia
(Kutoka 30:18)
8 fAkatengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kutoka kwa vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu pale ingilio la Hema la Kukutania.Ua Wa Hema La Kukutania
(Kutoka 27:9-19)
9 gKisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, ▼▼ Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.
na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 12Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini ▼▼ Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, pia ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano ▼▼ Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.
yalikuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio la ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. 17Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha. 18 kPazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano, 19likiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, na ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. 20 lVigingi vyote vya maskani na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba. Vifaa Vilivyotumika
21 mIfuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Musa, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Haruni. 22 n(Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu Bwana alichomwamuru Musa, 23 oakiwa pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, fundi stadi wa kutia nakshi, kubuni michoro, mtarizi kwa rangi ya buluu, ya zambarau, nyekundu na kitani safi.) 24 pJumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730, ▼▼ Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja.
kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 25 rFedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775, ▼▼ Talanta 100 na shekeli 1,775 za fedha ni sawa na tani 3.4.
kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 26 tKila mtu alitoa beka moja, ambayo ni sawa na nusu shekeli ya fedha, kwa kazi ya mahali patakatifu, kutoka kwa kila mtu aliyekuwa amehesabiwa mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, ambao jumla yao walikuwa wanaume 603,550. 27 uTalanta hizo 100 za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani, talanta moja kwa kila kitako. 28Akatumia zile shekeli hizo 1,775 kutengeneza kulabu za nguzo, kufunika ncha za nguzo na kutengeneza vitanzi vyake. 29Shaba iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa ilikuwa na uzito wa talanta 70 na shekeli 2,400. ▼▼ Talanta 70 na shekeli 2,400 ni sawa na tani 2.4.
30Akaitumia hiyo shaba kutengeneza vitako vya ingilio la Hema la Kukutania, madhabahu ya shaba pamoja na ule wavu wake na vyombo vyake vyote, 31 wvile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka.
Copyright information for
SwhKC