Isaiah 2:1-6

Mlima Wa Bwana

(Mika 4:1-3)

1 aHili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:

2 bKatika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa
kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote,
utainuliwa juu ya vilima,
na mataifa yote yatamiminika huko.

3 cMataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana,
kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.
Atatufundisha njia zake,
ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”
Sheria itatoka Sayuni,
neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

4 dAtahukumu kati ya mataifa
na ataamua migogoro ya mataifa mengi.
Watafua panga zao ziwe majembe,
na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.
Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,
wala hawatajifunza vita tena.


5 eNjooni, enyi nyumba ya Yakobo,
tutembeeni katika nuru ya Bwana

Siku Ya Bwana


6 fUmewatelekeza watu wako,
nyumba ya Yakobo.
Wamejaa ushirikina utokao Mashariki,
wanapiga ramli kama Wafilisti
na wanashikana mikono na wapagani.
Copyright information for SwhKC