Isaiah 57:3-8


3 a“Lakini ninyi:
Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,
ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!

4 bMnamdhihaki nani?
Ni nani mnayemcheka kwa dharau,
na kumtolea ndimi zenu?
Je, ninyi si watoto wa waasi,
uzao wa waongo?

5 cMnawaka tamaa katikati ya mialoni
na chini ya kila mti uliotanda matawi;
mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde
na chini ya majabali yenye mianya.


6 d“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu;
hizo ndizo sehemu yenu.
Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji,
na kutoa sadaka za nafaka.
Katika haya yote,
niendelee kuona huruma?

7 eUmeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka,
huko ulikwenda kutoa dhabihu zako.

8 fNyuma ya milango yako na miimo yako
umeweka alama zako za kipagani.
Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako,
umepanda juu yake na kukipanua sana;
ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao,
nawe uliangalia uchi wao.
Copyright information for SwhKC