Job 29
Ayubu Anamaliza Utetezi Wake
1 aAyubu akaendelea na hoja yake, akasema:2 b“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita,
zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,
3 cwakati taa yake iliniangazia kichwani changu,
na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!
4 dNatamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu,
wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,
5 ewakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami,
nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka,
6 fwakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi,
nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.
7 g“Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji
na kuketi katika kiwanja,
8 hvijana waliniona wakakaa kando,
nao wazee walioketi wakasimama;
9 iwakuu wakaacha kuzungumza
na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao;
10 jwenye vyeo wakanyamazishwa,
nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao.
11 kYeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu,
nao walioniona walinisifu,
12 lkwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,
naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
13 mMtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,
nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
14 nNiliivaa haki kama vazi langu;
uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
15 oNilikuwa macho ya kipofu
na miguu kwa kiwete.
16 pNilikuwa baba kwa mhitaji;
nilimtetea mgeni.
17 qNiliyavunja meno makali ya waovu,
na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
18 r“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe,
nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.
19 sMizizi yangu itafika mpaka kwenye maji,
nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.
20 tUtukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu,
upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’
21 u“Watu walinisikiliza kwa tumaini,
wakingojea ushauri wangu kwa utulivu.
22 vBaada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi;
maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini.
23 Waliningojea kama manyunyu ya mvua
na kuyapokea maneno yangu
kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli.
24 Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha;
nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao.
25 wNiliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao;
niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake;
nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.
Copyright information for
SwhKC