Leviticus 18:1-6

Uhusiano Wa Kukutana Kimwili Kinyume Cha Sheria

1 Bwana akamwambia Musa, 2 a“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wenu. 3 bMsifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao. 4 cNi lazima mzitii sheria zangu, na mwe waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wenu. 5 dZishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Bwana.

6“ ‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana.

Copyright information for SwhKC