Psalms 100
Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu
(Zaburi Ya Shukrani)
1 aMpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.2 bMwabuduni Bwana kwa furaha;
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3 cJueni kwamba Bwana ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
4 dIngieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5 eKwa maana Bwana ni mwema
na upendo wake wadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
Copyright information for
SwhKC