Psalms 111
Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu
1 ▼
▼ Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bMsifuni Bwana.Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote,
katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
2 cKazi za Bwana ni kuu,
wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3 dKazi zake zimejaa fahari na utukufu,
haki yake hudumu daima.
4 eAmefanya maajabu yake yakumbukwe,
Bwana ni mwenye neema na huruma.
5 fHuwapa chakula wale wanaomcha,
hulikumbuka agano lake milele.
6 gAmewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,
akiwapa nchi za mataifa mengine.
7 hKazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,
mausia yake yote ni ya kuaminika.
8 iZinadumu milele na milele,
zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9 jAliwapa watu wake ukombozi,
aliamuru agano lake milele:
jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10 kKumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.
Copyright information for
SwhKC