Psalms 120
Kuomba Msaada
(Wimbo Wa Kwenda Juu)
1 aKatika dhiki yangu namwita Bwana,
naye hunijibu.
2 bEe Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
3 Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4 cAtakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5 dOle wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6 Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7 Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema, wao wanataka vita.
Copyright information for
SwhKC