Psalms 122
Sifa Kwa Yerusalemu
(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi)
1 aNilishangilia pamoja na wale walioniambia,
“Twende nyumbani ya Bwana.”
2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama
malangoni mwako.
3 bYerusalemu imejengwa vyema kama mji
ambao umeshikamanishwa pamoja.
4 cHuko ndiko makabila hukwea,
makabila ya Bwana,
kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo
waliopewa Israeli.
5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,
viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
6 dOmba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:
“Wote wakupendao na wawe salama.
7 eAmani na iwepo ndani ya kuta zako
na usalama ndani ya ngome zako.”
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,
nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
9 fKwa ajili ya nyumba ya Bwana Mwenyezi Mungu wetu,
nitatafuta mafanikio yako.
Copyright information for
SwhKC