Psalms 131
Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu
(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi.)
1 aMoyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana,
macho yangu hayajivuni;
sijishughulishi na mambo makuu kunizidi
wala mambo ya ajabu mno kwangu.
2 bLakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.
3 cEe Israeli, mtumaini Bwana
tangu sasa na hata milele.
Copyright information for
SwhKC