Psalms 24
Mfalme Mkuu
(Zaburi Ya Daudi)
1 aDunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake,
ulimwengu, na wote waishio ndani yake,
2 bmaana aliiwekea misingi yake baharini
na kuifanya imara juu ya maji.
3 cNani awezaye kuupanda mlima wa Bwana?
Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?
4 dNi yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,
yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake
au kuapa kwa kitu cha uongo.
5 eHuyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana,
na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.
6 fHiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao,
wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7 gInueni vichwa vyenu, enyi malango,
inukeni enyi milango ya kale,
ili mfalme wa utukufu apate kuingia.
8 hNi nani huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Bwana aliye na nguvu na uweza,
ni Bwana aliye hodari katika vita.
9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
viinueni juu enyi milango ya kale,
ili Mfalme wa utukufu apate kuingia.
10 iNi nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;
yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Copyright information for
SwhKC