Psalms 29:3-8


3 aSauti ya Bwana iko juu ya maji;
Mungu wa utukufu hupiga radi,
Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.


4 bSauti ya Bwana ina nguvu;
sauti ya Bwana ni tukufu.

5 cSauti ya Bwana huvunja mierezi;
Bwana huvunja vipande vipande
mierezi ya Lebanoni.

6 dHufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,
Sirioni
Yaani Mlima Hermoni.
urukaruke kama mwana nyati.

7 fSauti ya Bwana hupiga kwa miali
ya umeme wa radi.

8 gSauti ya Bwana hutikisa jangwa;
Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
Copyright information for SwhKC