Romans 1:1-6

1 aPaulo, mtumishi wa Al-Masihi Isa, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu, 2 bInjili ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika Maandiko Matakatifu, 3 cyaani, Injili inayomhusu Mwanawe, yeye ambaye kwa uzao wa mwili alikuwa mzao wa Daudi, 4 dna ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, yaani, Isa Al-Masihi, Bwana wetu. 5 eKwa kupitia kwake na kwa ajili ya Jina lake, tumepokea neema na utume ili kuwaita watu miongoni mwa watu wa mataifa yote, waje kwenye utii utokanao na imani. 6 fNinyi nyote pia mko miongoni mwa watu walioitwa ili mpate kuwa mali ya Isa Al-Masihi.

Copyright information for SwhKC