Ephesians 6:10-15

10 aHatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 bVaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 12 cKwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 dKwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 14 eKwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 fnayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani.
Copyright information for SwhKC