Exodus 40:21-26

21 aKisha Musa akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Bwana alivyomwagiza.

22 bMusa akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia 23 cna kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

24 dAkaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu 25 ena kuziweka taa mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

26 fMusa akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia
Copyright information for SwhKC