‏ Ezekiel 2:1-6

Wito Wa Ezekieli

1 aAkaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 2 bAlipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami.

3 cAkaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. 4 dWatu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, ‘Hivi ndivyo anavyosema Bwana Mwenyezi.’ 5 eKama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. 6 fNawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao, usiogope, ingawa michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ingawa wao ni nyumba ya uasi.
Copyright information for SwhKC