Genesis 17:17-22

17 aIbrahimu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 18 bIbrahimu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”

19 cNdipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaka.
Isaka maana yake Kucheka.
Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.
20 eKwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. 21 fLakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” 22 gWakati alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Ibrahimu.

Copyright information for SwhKC