Judges 5:1-6

Wimbo Wa Debora

1 aNdipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:
2 b“Wakuu katika Israeli wanapoongoza,
wakati watu wanapojitoa
kwa hiari yao wenyewe:
mhimidini Bwana!


3 c“Sikieni hili, enyi wafalme!
Sikilizeni, enyi watawala!
Nitamwimbia Bwana, nitaimba;
kwa wimbo nitamhimidi Bwana,
Mungu wa Israeli.


4 d“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri,
ulipopita katika mashamba ya Edomu,
nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,
naam, mawingu yakamwaga maji.

5 eMilima ilitetemeka mbele za Bwana,
hata ule wa Sinai,
mbele za Bwana,
Mungu wa Israeli.


6 f“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,
katika siku za Yaeli,
barabara kuu hazikuwa na watu;
wasafiri walipita njia za kando.
Copyright information for SwhKC