Psalms 45:8-13


8 aMavazi yako yote yana harufu nzuri
ya manemane, udi na mdalasini;
kutoka kwenye majumba ya kifalme
yaliyopambwa kwa pembe za ndovu,
sauti za vinanda vya nyuzi
zinakufanya ufurahi.

9 bBinti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa;
kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.


10 cSikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio:
Sahau watu wako na nyumba ya baba yako.

11 dMfalme ameshangazwa na uzuri wako;
mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako.

12 eBinti wa Tiro atakuletea zawadi,
watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako.


13 fUtukufu wote una binti mfalme katika chumba chake;
vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.
Copyright information for SwhKC