1 Chronicles 8
Ukoo Wa Sauli Mbenyamini
1 aBenyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,
2Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
3 bWana wa Bela walikuwa:
Adari, Gera, Abihudi, 4 cAbishua, Naamani, Ahoa, 5Gera, Shefufani na Huramu.
6 dHawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
7Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
8Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara. 9Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. 11Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
12 eWana wa Elpaali walikuwa:
Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka), 13 fna Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
14Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15Zebadia, Aradi, Ederi, 16Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
17Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
19Yakimu, Zikri, Zabdi, 20Elienai, Silethai, Elieli, 21Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
22Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, 23Abdoni, Zikri, Hanani, 24Hanania, Elamu, Anthothiya, 25Ifdeya na Penueli.
26Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
28Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
29 gYeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.
Mke wake aliitwa Maaka. 30Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 31 hGedori, Ahio, Zekeri, 32na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
33 iNeri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
34 jYonathani akamzaa:
Merib-Baali, ▼ naye Merib-Baali akamzaa Mika.
35Wana wa Mika walikuwa:
Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.
36Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 37Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
38Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:
Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.
39Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:
Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 40 lWana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.
Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.
Copyright information for
SwhNEN