a Mwa 13:16; 15:5; 17:2-4; 18:18; 22:17; 24:1, 35; 25:11; 26:3, 4; 28:3, 4, 14; 24:1, 35; 25:11; 32:12; 35:11; 41:49; 47:27; 48:16-19; 22:18; Kut 1:7; 5:5; 32:13; 20:24; Kum 1:10; 10:22; 13:17; 26:5; Yos 11:4; 24:3; 2Sam 17:11; 1Fal 3:8; 4:20; 1Nya 27:23; 2Nya 1:9; Neh 9:23; Za 107:38; 67:6; 115:12; Isa 6:13; 10:22; 48:19; 51:2; 54:3; 60:22; 19:24; Yer 4:2; 33:22; Mik 4:7; Hes 22:12; 23:8, 20; 24:9; Isa 44:3; 61:9; 65:23; Mal 3:12; Hag 2:19; Zek 8:13
b Mwa 27:29; 15:5; 18:18; 22:18; 26:4; 28:4, 14; Kut 23:22; Hes 24:9; Kum 30:7; 9:5; Za 72:17; Isa 19:25; Mdo 3:25; Gal 3:8
e Ebr 11:9; 1Fal 12:1; Mwa 10:18; 33:18; 17:12; 35:4; Yos 17:7; 20:7; 24:26; Amu 7:1; 9:6; 8:31; 21:19; Za 60:6; 108:7
fMwa 8:20; 17:1, 8; 18:1; 26:2; 35:1; 13:4, 15-17; 15:18; 23:18; 24:7; 26:3-4; 28:13; 35:12; 48:4; 50:24; Kut 6:4-8; 6:3; 13:5, 11; 32:13; 33:1; Mdo 7:2, 5; Hes 10:29; 11:12; Kum 1:8; 2:31; 9:5; 11:9; 34:4; 30:5; Ebr 11:8; Rum 4:13; 2Fal 25:21; 1Nya 16:16; 2Nya 20:7; Za 109:9-11; Yer 25:5; Eze 47:14; Gal 3:16
Genesis 12
Wito Wa Abramu
1 Bwana akawa amemwambia Abramu, “Ondoka kutoka nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.2 a“Mimi nitakufanya taifa kubwa
na nitakubariki,
Nitalikuza jina lako,
nawe utakuwa baraka.
3 bNitawabariki wale wanaokubariki,
na yeyote akulaaniye nitamlaani;
na kupitia kwako mataifa yote duniani
yatabarikiwa.”
4 cHivyo Abramu akaondoka kama Bwana alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano. 5 dAbramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.
6 eAbramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo. 7 fBwana akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa akamjengea madhabahu Bwana aliyekuwa amemtokea.
8 gKutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea Bwana madhabahu na akaliitia jina la Bwana. 9 hKisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu.
Abramu Katika Nchi Ya Misri
10 iBasi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali. 11 jAlipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. 12Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai. 13 kSema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.”14Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura. 15Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akapelekwa kwa nyumba ya mfalme. 16 lKwa ajili ya Sarai, Farao akamtendea Abramu mema, naye Abramu akapata kondoo, ngʼombe, punda, ngamia na watumishi wa kiume na wa kike.
17 mLakini Bwana akamwadhibu Farao na nyumba yake kwa maradhi ya kufisha kwa sababu ya kumchukua Sarai, mke wa Abramu. 18 nNdipo Farao akamwita Abramu, akamuuliza, “Umenifanyia nini? Kwa nini hukuniambia ni mke wako? 19 oKwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!” 20Kisha Farao akawapa watu wake amri kuhusu Abramu, wakamsindikiza pamoja na mke wake na kila alichokuwa nacho.
Copyright information for
SwhNEN