‏ Isaiah 25:4-9

4 aUmekuwa kimbilio la watu maskini,
kimbilio la mhitaji katika taabu yake,
hifadhi wakati wa dhoruba
na kivuli wakati wa hari.
Kwa maana pumzi ya wakatili
ni kama dhoruba ipigayo ukuta
5 bna kama joto la jangwani.
Wewe wanyamazisha makelele ya wageni;
kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu,
ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.

6 cJuu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa
karamu ya vinono kwa mataifa yote,
karamu ya mvinyo wa zamani,
nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.
7 dJuu ya mlima huu ataharibu
sitara ihifadhiyo mataifa yote,
kile kifuniko kifunikacho mataifa yote,
8 eyeye atameza mauti milele.
Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;
ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.
Bwana amesema hili.

9 fKatika siku ile watasema,
“Hakika huyu ndiye Mungu wetu;
tulimtumaini, naye akatuokoa.
Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini;
sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”
Copyright information for SwhNEN