‏ Proverbs 7

Onyo Dhidi Ya Mwanamke Mzinzi

1 aMwanangu, shika maneno yangu
na kuzihifadhi amri zangu ndani yako.
2 bShika amri zangu nawe utaishi;
linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3 cYafunge katika vidole vyako;
yaandike katika kibao cha moyo wako.
4Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,”
uite ufahamu jamaa yako;
5 dwatakuepusha na mwanamke mzinzi,
kutokana na mwanamke mpotovu
na maneno yake ya kubembeleza.

6Kwenye dirisha la nyumba yangu
nilitazama nje kupitia upenyo
kwenye mwimo wa dirisha.
7 eNiliona miongoni mwa wajinga,
nikagundua miongoni mwa wanaume vijana,
kijana asiye na akili.
8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake,
akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9 fwakati wa machweo, jua likipungua nuru yake,
giza la usiku lilipokuwa likiingia.

10 gNdipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,
hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11 h(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,
miguu yake haitulii nyumbani;
12 imara kwenye barabara za mji,
mara kwenye viwanja vikubwa,
kwenye kila pembe huvizia.)
13 jHuyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,
na kwa uso usio na haya akamwambia:

14 k“Nina sadaka za amani nyumbani;
leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;
nimekutafuta na nimekupata!
16 lNimetandika kitanda changu
kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17 mNimetia manukato kitanda changu
kwa manemane, udi na mdalasini.
18 nNjoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;
tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19Mume wangu hayupo nyumbani;
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha
na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

21 oKwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;
alimshawishi kwa maneno yake laini.
22 pMara huyo kijana alimfuata yule mwanamke
kama fahali aendaye machinjoni,
kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23 qmpaka mshale umchome ini lake,
kama ndege anayenaswa kwenye mtego,
bila kujua itamgharimu maisha yake.

24 rSasa basi wanangu, nisikilizeni;
sikilizeni kwa makini nisemalo.
25 sUsiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,
wala usitangetange katika mapito yake.
26 tAliowaangusha ni wengi;
aliowachinja ni kundi kubwa.
27 uNyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,
Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.
Copyright information for SwhNEN