‏ Psalms 48

Sayuni, Mji Wa Mungu

Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora.

1 a Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,
katika mji wa Mungu wetu,
mlima wake mtakatifu.
2 bNi mzuri katika kuinuka kwake juu sana,
furaha ya dunia yote.
Kama vilele vya juu sana vya Safoni
Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini.
ni Mlima Sayuni,
mji wa Mfalme Mkuu.
3 dMungu yuko katika ngome zake;
amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.

4 eWakati wafalme walipounganisha nguvu,
waliposonga mbele pamoja,
5 fwalimwona nao wakashangaa,
wakakimbia kwa hofu.
6 gKutetemeka kuliwashika huko,
maumivu kama ya mwanamke
mwenye utungu wa kuzaa.
7 hUliwaangamiza kama meli za Tarshishi
zilizovunjwa na upepo wa mashariki.

8 iKama tulivyokuwa tumesikia,
ndivyo tulivyoona
katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote,
katika mji wa Mungu wetu:
Mungu ataufanya uwe salama milele.

9 jEe Mungu, hekaluni mwako
tunatafakari upendo wako usiokoma.
10 kEe Mungu, kama jina lako lilivyo,
sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia,
mkono wako wa kuume umejazwa na haki.
11 lMlima Sayuni unashangilia,
vijiji vya Yuda vinafurahi
kwa sababu ya hukumu zako.

12 mTembeeni katika Sayuni,
uzungukeni mji,
hesabuni minara yake;
13 nyatafakarini vyema maboma yake,
angalieni ngome zake,
ili mpate kusimulia habari zake
kwa kizazi kijacho.
14 oKwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele;
atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.
Copyright information for SwhNEN