g Za 3:4; 4:3; 27:5; 50:15; 94:13; 80:18; 91:15; Isa 30:19; 58:9; 65:24; Ay 22:27; Zek 13:9; Hab 3:16
Psalms 86
Kuomba Msaada
Maombi ya Daudi.
1 aEe Bwana, sikia na unijibu,kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
2 bLinda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako,
wewe ni Mungu wangu,
mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3 cEe Bwana, nihurumie mimi,
kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4 dMpe mtumishi wako furaha,
kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana,
ninainua nafsi yangu.
5 eEe Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe,
umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6 fEe Bwana, sikia maombi yangu,
sikiliza kilio changu unihurumie.
7 gKatika siku ya shida yangu nitakuita,
kwa maana wewe utanijibu.
8 hEe Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe,
hakuna matendo ya kulinganishwa na yako.
9 iEe Bwana, mataifa yote uliyoyafanya
yatakuja na kuabudu mbele zako;
wataliletea utukufu jina lako.
10 jKwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu;
wewe peke yako ndiwe Mungu.
11 kEe Bwana, nifundishe njia yako,
nami nitakwenda katika kweli yako;
nipe moyo usiositasita,
ili niweze kulicha jina lako.
12 lEe Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote;
nitaliadhimisha jina lako milele.
13 mKwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;
umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi. ▼
▼Yaani Kuzimu.
14 oEe Mungu, wenye majivuno wananishambulia;
kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu:
watu wasiokuheshimu wewe.
15 pLakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,
si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
16 qNigeukie na unihurumie;
mpe mtumishi wako nguvu zako,
mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike. ▼
▼Au: mwokoe mwanao mwaminifu.
17 sNipe ishara ya wema wako,
ili adui zangu waione nao waaibishwe,
kwa kuwa wewe, Ee Bwana,
umenisaidia na kunifariji.
Copyright information for
SwhNEN