Jeremiah 2:5-7
5 aHivi ndivyo asemavyo Bwana:“Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu,
hata wakatangatanga mbali nami hivyo?
Walifuata sanamu zisizofaa,
nao wenyewe wakawa hawafai.
6 bHawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana,
aliyetupandisha kutoka Misri
na kutuongoza kupitia nyika kame,
kupitia nchi ya majangwa na mabonde,
nchi ya ukame na giza,
nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake
wala hakuna mtu aishiye humo?’
7 cNiliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu
ili mpate kula matunda yake
na utajiri wa mazao yake.
Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu,
na kuufanya urithi wangu chukizo.
Copyright information for
SwhNEN