Micah 6:1-5
Shauri La Bwana Dhidi Ya Israeli
1 aSikiliza asemalo Bwana:“Simama, tetea shauri lako mbele ya milima;
vilima na visikie lile unalotaka kusema.
2 bSikilizeni, ee milima, mashtaka ya Bwana,
sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia.
Kwa kuwa Bwana ana shauri dhidi ya watu wake;
anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.
3 c“Watu wangu, nimewatendea nini?
Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu.
4 dNimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa
kutoka nchi ya utumwa.
Nilimtuma Mose awaongoze,
pia Aroni na Miriamu.
5 eWatu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu
alivyofanya shauri
na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu.
Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali,
ili mfahamu matendo ya haki ya Bwana.”
Copyright information for
SwhNEN