‏ Proverbs 19

1 aAfadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,
kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.

2 bSio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa,
wala kufanya haraka na kuikosa njia.

3 cUpumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake
hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana.

4 dMali huleta marafiki wengi,
bali rafiki wa mtu maskini humwacha.

5 eShahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo hataachwa huru.

6 fWengi hujipendekeza kwa mtawala
na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.

7 gMtu maskini huepukwa na ndugu zake wote:
Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani!
Ingawa huwafuata kwa kuwasihi,
hawapatikani popote.

8 hYeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,
yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.

9 iShahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo ataangamia.

10 jHaistahili mpumbavu kuishi katika anasa,
itakuwa vibaya kiasi gani
kwa mtumwa kuwatawala wakuu.

11 kHekima ya mtu humpa uvumilivu,
ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.

12 lGhadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba,
bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.

13 mMwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye,
naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

14 nNyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,
bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

15 oUvivu huleta usingizi mzito,
naye mtu mzembe huona njaa.

16 pYeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake,
bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.

17 qYeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana,
naye atamtuza kwa aliyotenda.

18 rMrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini,
usiwe mshirika katika mauti yake.

19Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake,
kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena.

20 sSikiliza mashauri na ukubali mafundisho,
nawe mwishoni utakuwa na hekima.

21 tKuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,
lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.

22Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,
afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.

23 uKumcha Bwana huongoza kwenye uzima,
kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,
bila kuguswa na shida.

24 vMtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!

25 wMpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara,
mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa.

26 xYeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake
ni mwana aletaye aibu na fedheha.

27 yMwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,
utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.

28 zShahidi mla rushwa hudhihaki hukumu
na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi.

29 aaAdhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka
na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.
Copyright information for SwhNEN