‏ Psalms 115

Mungu Mmoja Wa Kweli

1 aSio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.

2 bKwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
3 cMungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
4 dLakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5 eZina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8 fWale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.

9 gEe nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
10 hEe nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
11 iNinyi mnaomcha, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.

12 j Bwana anatukumbuka na atatubariki:
ataibariki nyumba ya Israeli,
ataibariki nyumba ya Aroni,
13 katawabariki wale wanaomcha Bwana,
wadogo kwa wakubwa.

14 l Bwana na awawezeshe kuongezeka,
ninyi na watoto wenu.
15 mMbarikiwe na Bwana
Muumba wa mbingu na dunia.

16 nMbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana,
lakini dunia amempa mwanadamu.
17 oSio wafu wanaomsifu Bwana,
wale washukao mahali pa kimya,
Mahali pa kimya maana yake ni Kuzimu, yaani Sheol kwa Kiebrania.

18 qbali ni sisi tunaomtukuza Bwana,
sasa na hata milele.

Msifuni Bwana.
Msifuni Bwana ni Kiebrania Hallelu Yah.

Copyright information for SwhNEN