Psalms 133
Sifa Za Pendo La Undugu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1 aTazama jinsi ilivyo vyema na kupendezawakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
2 bNi kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.
3 cNi kama vile umande wa Hermoni
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake,
naam, hata uzima milele.
Copyright information for
SwhNEN