‏ Psalms 17

Sala Ya Mtu Asiye Na Hatia

Sala ya Daudi.

1 aSikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki,
sikiliza kilio changu.
Tega sikio kwa ombi langu,
halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.
2 bHukumu yangu na itoke kwako,
macho yako na yaone yale yaliyo haki.

3 cIngawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku,
ingawa umenijaribu, hutaona chochote.
Nimeamua kwamba kinywa changu
hakitatenda dhambi.
4 dKuhusu matendo ya wanadamu:
kwa neno la midomo yako,
nimejiepusha
na njia za wenye jeuri.
5 eHatua zangu zimeshikamana na njia zako;
nyayo zangu hazikuteleza.

6 fEe Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu,
nitegee sikio lako na usikie ombi langu.
7 gUonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu,
wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume
wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.
8 hNilinde kama mboni ya jicho lako,
unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako
9 ikutokana na waovu wanaonishambulia,
kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

10 jHuifunga mioyo yao iliyo migumu,
vinywa vyao hunena kwa majivuno.
11 kWamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira,
wakiwa macho, waniangushe chini.
12 lWamefanana na simba mwenye njaa awindaye,
kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.

13 mInuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe,
niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.
14 nEe Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii,
kutokana na watu wa ulimwengu huu
ambao fungu lao liko katika maisha haya.

Na wapate adhabu ya kuwatosha.
Watoto wao na wapate zaidi ya hayo,
hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.
15 oNa mimi katika haki nitauona uso wako,
niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.
Copyright information for SwhNEN