‏ Psalms 23

Bwana Mchungaji Wetu

Zaburi ya Daudi.

1 a Bwana ndiye mchungaji wangu,
sitapungukiwa na kitu.
2 bHunilaza katika malisho
ya majani mabichi,
kando ya maji matulivu huniongoza,
3 chunihuisha nafsi yangu.
Huniongoza katika njia za haki
kwa ajili ya jina lake.
4 dHata kama nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.

5 eWaandaa meza mbele yangu
machoni pa adui zangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
kikombe changu kinafurika.
6 fHakika wema na upendo vitanifuata
siku zote za maisha yangu,
nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
milele.
Copyright information for SwhNEN