‏ Psalms 30

Maombi Ya Shukrani

Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.

1 aNitakutukuza wewe, Ee Bwana,
kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
2 bEe Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
3 cEe Bwana, umenitoa Kuzimu,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

4 dMwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;
lisifuni jina lake takatifu.
5 eKwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,
bali upendo wake hudumu siku zote.
Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,
lakini asubuhi kukawa na furaha.

6 fNilipofanikiwa nilisema,
“Sitatikiswa kamwe.”
7 gEe Bwana, uliponijalia,
uliuimarisha mlima wangu,
lakini ulipouficha uso wako
nilifadhaika.

8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita,
kwa Bwana niliomba rehema:
9 h“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu?
Katika kushuka kwangu shimoni?
Je, mavumbi yatakusifu?
Je, yatatangaza uaminifu wako?
10 iEe Bwana, unisikie na kunihurumia,
Ee Bwana, uwe msaada wangu.”

11 jUligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,
ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,
12 kili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.
Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.
Copyright information for SwhNEN