‏ Psalms 33

Ukuu Na Wema Wa Mungu

1 aMwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki;
kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2 bMsifuni Bwana kwa kinubi,
mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.
3 cMwimbieni wimbo mpya;
pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.

4 dMaana neno la Bwana ni haki na kweli,
ni mwaminifu kwa yote atendayo.
5 e Bwana hupenda uadilifu na haki;
dunia imejaa upendo wake usiokoma.

6 fKwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,
jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.
7 gAmeyakusanya maji ya bahari
kama kwenye chungu;
vilindi vya bahari
ameviweka katika ghala.
8 hDunia yote na imwogope Bwana,
watu wote wa dunia wamche.
9 iKwa maana Mungu alisema, na ikawa,
aliamuru na ikasimama imara.
10 j Bwana huzuia mipango ya mataifa,
hupinga makusudi ya mataifa.
11 kLakini mipango ya Bwana inasimama imara milele,
makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.

12 lHeri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake.
13 mKutoka mbinguni Bwana hutazama chini
na kuwaona wanadamu wote;
14 nkutoka maskani mwake huwaangalia
wote wakaao duniani:
15 oyeye ambaye huumba mioyo yao wote,
ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.
16 pHakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake;
hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake.
17 qFarasi ni tumaini la bure kwa wokovu,
licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa.
18 rLakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao,
kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,
19 sili awaokoe na mauti,
na kuwahifadhi wakati wa njaa.

20 tSisi tunamngojea Bwana kwa matumaini,
yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
21 uMioyo yetu humshangilia,
kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.
22 vUpendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana,
tunapoliweka tumaini letu kwako.
Copyright information for SwhNEN