‏ Psalms 50

Ibada Ya Kweli

Zaburi ya Asafu.

1 aMwenye Nguvu, Mungu, Bwana,
asema na kuiita dunia,
tangu mawio ya jua
hadi mahali pake liendapo kutua.
2 bKutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu,
Mungu anaangaza.
3 cMungu wetu anakuja na hatakaa kimya,
moto uteketezao unamtangulia,
akiwa amezungukwa na tufani kali.
4 dAnaziita mbingu zilizo juu,
na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake:
5 e“Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu,
waliofanya agano nami kwa dhabihu.”
6 fNazo mbingu zinatangaza haki yake,
kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu.

7 g“Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema,
ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu:
Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu.
8 hSikukemei kwa sababu ya dhabihu zako,
au sadaka zako za kuteketezwa,
ambazo daima ziko mbele zangu.
9 iSina haja ya fahali wa banda lako,
au mbuzi wa zizi lako.
10 jKwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu,
na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu.
11 kNinamjua kila ndege mlimani,
nao viumbe wa kondeni ni wangu.
12 lKama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi,
kwa maana ulimwengu ni wangu,
pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.
13Je, mimi hula nyama ya mafahali
au kunywa damu ya mbuzi?
14 mToa sadaka za shukrani kwa Mungu,
timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana,
15 nna uniite siku ya taabu;
nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”
16 oLakini kwake mtu mwovu, Mungu asema:

“Una haki gani kunena sheria zangu
au kuchukua agano langu midomoni mwako?
17 pUnachukia mafundisho yangu
na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18 qUnapomwona mwizi, unaungana naye,
unapiga kura yako pamoja na wazinzi.
19 rUnakitumia kinywa chako kwa mabaya
na kuuongoza ulimi wako kwa hila.
20 sWanena daima dhidi ya ndugu yako
na kumsingizia mwana wa mama yako.
21 tMambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya,
ukafikiri Mimi nami ni kama wewe.
Lakini nitakukemea
na kuweka mashtaka mbele yako.

22 u“Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu,
ama sivyo nitawararua vipande vipande,
wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa:
23 vAtoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi,
naye aiandaa njia yake
ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.”
Copyright information for SwhNEN