Psalms 59
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue.
1 a bEe Mungu, uniokoe na adui zangu,unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.
2 cUniponye na watu watendao mabaya,
uniokoe kutokana na wamwagao damu.
3 dTazama wanavyonivizia!
Watu wakali wananifanyia hila,
ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea
wala kutenda dhambi.
4 eSijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia.
Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya!
5 fEe Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli!
Zinduka uyaadhibu mataifa yote,
usionyeshe huruma kwa wasaliti.
6 gHurudi wakati wa jioni,
wakibweka kama mbwa,
wakiuzurura mji.
7 hTazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao,
hutema upanga kutoka midomo yao,
nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”
8 iLakini wewe, Bwana, uwacheke;
unayadharau mataifa hayo yote.
9 jEe nguvu yangu, ninakutazama wewe,
wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,
10Mungu wangu unipendaye.
Mungu atanitangulia,
naye atanifanya niwachekelee
wale wanaonisingizia.
11 kLakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu,
au sivyo watu wangu watasahau.
Katika uwezo wako wafanye watangetange
na uwashushe chini.
12 lKwa ajili ya dhambi za vinywa vyao,
kwa ajili ya maneno ya midomo yao,
waache wanaswe katika kiburi chao.
Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,
13 mwateketeze katika ghadhabu,
wateketeze hadi wasiwepo tena.
Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia
kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo.
14Hurudi jioni,
wakibweka kama mbwa,
wakiuzurura mji.
15 nWanatangatanga wakitafuta chakula,
wasipotosheka hubweka kama mbwa.
16 oLakini mimi nitaziimba nguvu zako,
asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;
kwa maana wewe ndiwe ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa shida.
17 pEe uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.
Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,
Mungu unipendaye.
Copyright information for
SwhNEN